UTAMADUNI & VIJANA: Kujiendeleza kupitia Utamaduni wetu
Kaunti ya Tana River ni tajiri katika mambo ya utamaduni. Hata wakoloni walitumia muda mrefu kutathmini na kuelewa utamaduni wetu ili waweze kuutumia katika kutawala sehemu zingine. Wimbo wa taifa wenyewe unatoka Tana River. Tuna turathi kadha wa kadha kutoka jamii zote-kuanzia wakulima, wafugaji, na hata wavuvi. Urith tuliopata kutoka kw amababu zetu haupatikani popote pengine ulimwenguni. Zaidi ya nusu ya idadi ya watu wetu ni vijana mahiri, wenye nguvu. Hata hivyo hizi nguvu hazijatumiwa vilivyo kufaidi jamii. Wanasiasa Wengi wa vijana hutumika vibaya wakati wa uchaguzi, kisha kusahaulika mara kura zinapohesabiwa. Ni wakati wa kubadilisha simulizi hiyo.
.

Ili kuwapa nafasi vijana wetu kuendelea kama sehemu zingine za nchi tunapanga kuweka HOTOSPOTS za bure sehemu kadha katika kila Sub-county ili waweze kutumia kuelewa dunia inapoelekea. Tunaamini kwamba watakapo elimishwa kutumia mbinu za kisasa, ga kutafuta soko za bidhaa zao, mabo yatabadilika. Siku hizi kazi na TENDER nyingi hutangazwa na kutolewa kwa mitandao. Bila kuwa na uwezo wa kuingia na kutafuta hizi kazi zinazowekwa mitandaoni, tutazidi kuachwa nyuma.
Pia tutakuwa na matukio ya kila mwaka kama SIKU YA UTAMADUNI ambapo shughuli za kitamaduni kama mashindano ya kuendesha mitumbwi, mchezo wa bao na mingeneo yatakuwa. Hassan Morowa amekuwa mstari wa mbele katika sherehe za JILLA ambayo hufanyika Nairobi kila mwaka. Siku hiyo waKenya hushuhudia tamaduni zetu kuanzia mavazi, vyakula nyimbo na michezo ya kwetu. Kaunti zingine kama Meru na Busia zimevutiwa na maonyesho hayo na wameonyesha nia ya kuja kusoma namna maandalizi hayo yanavyofanyika kwa nia ya kuyaiga au kushirikiana nasi, Kwa hakika yajayo yanapendeza kiutamaduni pindi Hassan atakapochaguliwa kama gavana.

