top of page
DONATE

BADO YANAPENDEZA. YAJAYO YATAFURAHISHA.

“Sauti Yako ndio Ahadi Yetu”

.

Sauti yako ndiyo iliyonivuta kama smaku kuwania kiti cha Ugavana. Mahitaji yenu ndiyo yalionipa motisha ya kujitwika mzigo wa kuiongoza Tana River kwa sababu:
Nia tunayo
Uwezo tunao
na mbinu tunazo.

Karibu tuijenge Tana River yetu,
bila ubaguzi.
Ngoja ngoja, matumbo huoza
Kuna haja, sisi kuongoza
Si vioja, watu kupoteza
Mwenye koja, ni Mola Muweza

Hatutagawanywa tena kwa misingi ya kikabila, dini, tabaka, mipaka wala kukaa kimya.

Twasema pamoja, si kusemewa
Twapanga pamoja, si kupangiwa
Twajenga pamoja, si kujengewa

|

  • Facebook
  • TikTok
  • YouTube
  • Twitter
  • Instagram
DSC_1335 crop.JPG

DSC_1193_edited.png

.

KUNIHUSU

“Kutumia Uwezo wangu kuleta mabadiliko”

Hili si jambo langu bali ni jambo letu. Kila sauti ya mwanaTana kutoka kila kijiji inahitajika, kila matarajio, kila mbinu inafaa kutumiwa kuibadilisha Kaunti yetu. Tunajenga umma ulio na mvuto kuzidi siasa yenyewe. Tumezowea siasa za udanganyifu na kukubali wanasiasa kutumia mbinu fiche za kutugawanya ili lao liwaendee wakituwacha kwa mataa. Tunaubadilisha mfumo huu. Huu ni mwamko mpya. Tutaleta huduma kwa jamii bila kubagua kabila, dini wala tabaka. Njoo tusaidiane kuubadilisha mustakbali wa Tana River yetu. Sisi ni watu wa kuigwa sio wa kuiga.

Tujenge kaunti pamoja.  Niaminini ninayosema.... Kwa ushirikiano wenu nitatumia tajriba yangu ya miongo kadhaa, niliyoipata kwa kufanya kazi kwenye mabenki makubwa makubwa, biashara na kuamiliana na watu mashuhuri ndani na nje ya nchi ili kugeuza miundo misingi na miundo mbinu ya kuleta maendeleo ya kuonekana na wala sio ya domo kaya. Mimi nimesomea masomo ya uchumi kama alivyosomea raisi wetu wa tatu hayati Kibaki. Na tumeona alivyoibadilisha Kenya. Nipeni nafasi nami niibadilishe Tana River kupitia mawazo na matarajio yenu. Nia? Nia ni kuifanya kaunti yetu iwe kielelezo kikubwa kwa kaunti zingine waweze kuiga. Na tunaanza kwa kuifanya Tana River kuwa breadbasket ya Kenya. Yaani, iwe sisi ndio wa kuilisha Kenya nzima. Na hilo si ajabu, linawezekana.

  • Facebook
  • TikTok
  • YouTube
  • Twitter
  • Instagram

JIUNGE NASI

Karibu tuijenge Tanariver. Njoo hapa.

bottom of page