top of page
DONATE

UWIANO: Uti Wa Mgongo Wa Maendeleo Yetu

Usalama ni muhimu sana katika mpango mzima wa maendeleo. Tumeshuhudia watu wetu ambao ni mahiri kibiashara na usomi wakikimbia kuekeza katika kaunti yetu. Badala yake hawa mahodari wetu huenda wakawekeza katika kaunti zingine. Kwa ajili hii akili za watu wetu hazitumiki kujenga kaunti yetu bali kujenga kaunti zingine.  Hali hii inahitaji kukomeshwa kwa uharaka. Wananchi wetu lazima wajisikie kuwa wako salama majumbani mwao, katika biashara zao, mashuleni, na barabarani mwetu, iwe mchana au usiku. Hapo ndipo maendeleo yatapatikana. Ndio maana serikali ya Hassan Morowa ikishirikiana na serikali kuu, itahakikisha usalama unadumishwa ili tuweze kupata maendeleo ya haraka.

Local law enforcement team ensuring peace during a community development dialogue tour by Hassan Morowa.

Mtazamo wetu ni kwamba gavana wa Tana River anayekuja ni lazima ahikikishe usalama unapatikana. Hassan Morowa kwa kushirikiana na serikali kuu atahakikisha kuna uwiano kati ya serikali kuu na county inspectorate kila inapowezekana. Kufanikisha hili kutakuwa na community policing ("sungusungu") na homeguards

Hassan atachagua wafanyakazi wa serikali walio na ujuzi ambao wako tayari kujitolea ili kuhakikisha kuwa manifesto yake inatekelezwa. Na nguzo ya kwanza ya manifesto yake (C.A.C.H.E) ndio hii ya COHESION.

bottom of page