top of page
DONATE

KILIMO: Ufunguo wa sisi kulisha Kenya nzima

Kaunti ya Tana River imebarikiwa kuwa na maliasili nyingi na ardhi yenye rutuba. Ni Kaunti pekee nchini Kenya ambayo jina lenyewe ni maliasili, Mto Tana, ambao ni mto wa kudumu na mkubwa zaidi nchini Kenya. Bidhaa za kilimo za Kaunti ya Tana river zimekuwa zikitamaniwa kibiashara kote ulimwenguni lakini bado hatujatumia uwezo huu kubadili maisha yetu. Bado tumegubikwa na uchochole na hali ngumu ya maisha.

River Tana. Our permanent tiver that will be central in making Tana River the bredbasket of Kenya

Food on the Table
Money in the Pocket

Hapa, tunazungumza juu ya hali halisi na kuepuka lile wanatana hukiita "Kizungu-mingi". Kwa mtu wa kawaida wa Tana River, anachohitaji ni chakula mezani na pesa mfukoni, khalas! Tana River imevutia wawekezaji wengi kutoka nchi za Ulaya na Uarabuni ambao wako tayari kubadilisha kaunti yetu. Hata hivyo, tunajua serikali ya Kaunti imekuwa kizingiti kikubwa kwa mambo kama haya. Kwetu sisi kama kaunti ni kama ambaye tunafurahia kulalamika kuwa "tunaonewa" ilhali kiuhalisia sisi ndio tunajiburuza. Kuna umuhimu wa haraka kubadilisha hali hii. Tukingojea hayo makubwa, tunapanga kupatiana pembejeo za kwa wakulima na kununua matrakta ya kukodi kwa bei rahisi ili kuuboresha ukulima wa walimi wadogo. Ikiwezekana kila familia iwe na eka zisizopungua kumi na matrakta ya kaunti yawe yanawalimia watu bure au kwa bei nafuu kwa masharti tutakayoweka sisi wenyewe.

 

Ni wakati wa kuanzisha au kukaribisha waekezaji kwetu. Uropa iliendelea kwa sababu ya kufungua viwanda vingi, kile walichokiita INDUSTRIALISATION. Baada ya kupata pembejeo, kuwa na ardhi isiyopungu ekari kumi kila familia na kulimiwa bure au kwa bei nafuu, tunatarajia mavuno kabambe kutokana na hali hii. Kuliko kusafirisha  haya mazao kwenda kwengine, ni bora kukaribisha viwanda viweze kununua na kutengeza bidha hukuhuku kwetu Tana River. Hii itapatiana fursa kwa vijana kupata kazi kuanzia kilimo chenyewe, kusafirisha, na ajira viwandani.


Akiwa gavana, Hassan Morowa atakuwa mstari wa mbele kuinua sekta ya kilimo, ufugaji na misitu ya Tana. Yeye kama mwana mshirika akiwa amefanya kazi kwa miaka mingi katika sekta ya ushirika, atazipa kipaumbele juhudi za kupanua mauzo ya nje na kufungua masoko mapya ya bidhaa za Tana River. Kwa kuzingatia ahadi yake ya kuifanya Tana ikue tena, Hassan ataunga mkono ukuaji wa sekta hizi mpya na muhimu kwa ukuzaji, ili kuhakikisha Tana River inalisha Kenya nzima. Huu ni wakati wa Tana River kuwa kielelezo kwa Kaunti zingine kuiga, sio sisi kuiga wengine daima dahari.

Hakika, tunatambua changamoto zinazowakumba watu wetu. Kwa miaka mingi tumekuwa tukitegemea mbinu za kilimo za jadi, na ukweli ni kwamba ni watu wachache sana waliofanikiwa katika kilimo. Huo ndio ukweli. Ingawa tuna maafisa wa kilimo (agricultural extension officers) wanaolipwa na serikali, ni wachache mno kati ya watu wetu wanaokubali kufuata ushauri unaotolewa na maafisa hao katika sekta ya kilimo na mifugo.

Kwa kiwango kikubwa, hii ndiyo sababu maisha yetu hayajabadilika kwa karne nyingi. Ingawa kiutamaduni tuna uwezo mkubwa wa kufanya kazi kwa pamoja, tunasita kutumia mtazamo huo katika kilimo. Tunastahabu kufanya kazi binafsi, na kwa sababu hiyo tunashindwa kabisa kufikia faida ya uzalishaji wa pamoja na kuongeza mapato kwa kiwango kikubwa.

Hili linahitaji kuangaziwa kwa haraka na wataalamu wetu pamoja na viongozi mashinani.

bottom of page